Katika hafla ya kiheshima iliyofanyika katika Mji Mtakatifu wa Najaf al-Ashraf, Ayatollah al-Udhma Abdullah Javadi Amoli alitunukiwa kwa kutambua mchango wake mkubwa katika nyanja za elimu na maarifa ya Kiislamu.

14 Mei 2025 - 14:58

Hafla ya Kiheshima ya Kumtunuku Ayatollah al-Udhma Abdullah Javadi Amoli imefanyika katika Haram Tukufu ya Imam Ali (a.s)

Kwa mujibu wa shirika la habari la kimataifa la AhlulBayt (a.s) -ABNA- Kitengo cha Masuala ya Kiakili na Kiutamaduni cha Atabatu Alawiyya kiliratibu sherehe hiyo yenye heshima kubwa kwa ajili ya kumuenzi na kumtukuza Ayatollah Javadi Amoli.

Katika tukio hilo, viongozi wa kidini, wasomi wa chuo, na wanafunzi wa seminari walihudhuria kwa wingi, wakionesha mshikamano wao wa kielimu na heshima kwa juhudi zisizochoka za Ayatollah Amoli katika kueneza mafundisho ya Qur’ani Tukufu na Ahlul Bayt (a.s).

Hafla ya Kiheshima ya Kumtunuku Ayatollah al-Udhma Abdullah Javadi Amoli imefanyika katika Haram Tukufu ya Imam Ali (a.s)

Hafla ya Kiheshima ya Kumtunuku Ayatollah al-Udhma Abdullah Javadi Amoli imefanyika katika Haram Tukufu ya Imam Ali (a.s)

Hafla hii ilifanyika kwa kuhudhuriwa na Sayyid Isa Kharsan, mlezi wa kidini wa Atabatu Alawiyya, pamoja na wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Haram hiyo, wakuu wa idara mbalimbali za Ataba, na umati mkubwa wa walimu na wanafunzi wa seminari ya Najaf al-Ashraf, sambamba na wahadhiri na wasomi kutoka vyuo vikuu.

Hafla ya Kiheshima ya Kumtunuku Ayatollah al-Udhma Abdullah Javadi Amoli imefanyika katika Haram Tukufu ya Imam Ali (a.s)

Hafla ya Kiheshima ya Kumtunuku Ayatollah al-Udhma Abdullah Javadi Amoli imefanyika katika Haram Tukufu ya Imam Ali (a.s)

Katika hafla hii, ambayo ililenga kutambua juhudi za kielimu na kiitikadi za Marjaa mkubwa wa Kishia, Ayatollah al-Udhma Javadi Amoli, wazungumzaji walisisitiza nafasi yake ya juu ya kielimu na mchango wake mkubwa katika kueneza maarifa ya Kiislamu na kukuza fikra za Ahlul Bayt (amani iwe juu yao).

Hafla ya Kiheshima ya Kumtunuku Ayatollah al-Udhma Abdullah Javadi Amoli imefanyika katika Haram Tukufu ya Imam Ali (a.s)

Hafla ya Kiheshima ya Kumtunuku Ayatollah al-Udhma Abdullah Javadi Amoli imefanyika katika Haram Tukufu ya Imam Ali (a.s)

Hafla hii ilifanyika katika mazingira yaliyojaa heshima na hali ya kiroho, na ilipokelewa kwa mapokezi makubwa na ya kuvutia kutoka kwa washiriki waliokuwepo.

Hafla ya Kiheshima ya Kumtunuku Ayatollah al-Udhma Abdullah Javadi Amoli imefanyika katika Haram Tukufu ya Imam Ali (a.s)

Hafla ya Kiheshima ya Kumtunuku Ayatollah al-Udhma Abdullah Javadi Amoli imefanyika katika Haram Tukufu ya Imam Ali (a.s)

Hafla ya Kiheshima ya Kumtunuku Ayatollah al-Udhma Abdullah Javadi Amoli imefanyika katika Haram Tukufu ya Imam Ali (a.s)

Atabatu Alawiyya Tukufu hapo awali pia imeandaa na kuwakaribisha maulamaa na wasomi kutoka ulimwengu wa Kiislamu, kwa lengo la kuonesha nafasi muhimu ya Marjaa wa Kishia katika kuimarisha misingi ya kielimu ya Umma wa Kiislamu.

Your Comment

You are replying to: .
captcha